Madhara ya Bawasir
Ikiwa haitatibiwa, bawasiri inaweza kusababisha madhara yafuata
1. Maumivu makali
Bawasiri hasa ya nje huweza kusababisha maumivu makali, hasa wakati wa kujisaidia.
Maumivu yanaweza kuwa ya kuungua au kuuma
2. Kutokwa damu
Moja ya dalili kuu ni kutokwa damu wakati wa kujisaidia.
Damu huwa nyekundu na safi.
Ikiwa hali hii itaendelea bila matibabu, inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini (anemia).
3. Kuwashwa na muwasho wa mara kwa mara
Eneo la puru huwa na muwasho mkali unaoleta usumbufu mkubwa.
Kuwashwa huku kunaweza kupelekea kuchubuka kwa ngozi na maambukizi.
4. Uvimbaji wa puru (anal swelling)
Mishipa iliyoathirika huvimba na kusababisha uvimbe wa puru, ambao huweza kuwa mgumu kurudi ndani baada ya kutoka.
Baadhi ya aina za bawasiri (hasa ya nje) huweza kuonekana kama vinundu vya nyama.
5. Kupata choo kigumu au kigumu kujisaidia
Maumivu na hofu ya kujisaidia hupelekea mtu kushikilia choo, na hivyo kuongeza ugumu wa tatizo.
Inaweza kuchangia kupata vidonda ndani ya puru
6. Maambukizi (Infections)
Mishipa iliyopasuka au kuchubuka inaweza kuruhusu vijidudu kuingia, na kusababisha maambukizi hatari.l
7. Thrombosed hemorrhoids (bawasiri yenye damu iliyoganda)
Hii ni hali ambapo damu huganda ndani ya uvimbe wa bawasiri na kusababisha maumivu makali sana, uvimbe mkubwa na hali ya dharura inayohitaji matibabu ya haraka
8. Kuvuja kwa kinyesi bila kujizuia (fecal incontinence)
Katika hali za muda mrefu au kali, bawasiri inaweza kuathiri misuli ya puru, na kusababisha mtu kutoweza kudhibiti haja ndogo au kubwa vizuri.

0 Comments